Mtu mmoja afariki kutokana na ugonjwa wa Kalazaar Marsabit, sita wakipokea matibabu kulingana na serikali ya kaunti.
February 21, 2025
Wabunge pamoja na wananchi wanapswa kumsikiza na kumsamehe naibu wa Rais Rigathi Gachagua ili kutuliza mgogoro utakaozuka iwapo Gachagua atang`atuliwa Mamlakani.
Haya ni kwa mujibu wa Harrison Mugo ambaye ni mwanachama wa kamati kuu ya chama cha kisiasa cha National Vision Party (NVP).
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee Mugo ameelezea kuwa ni wajibu wa kila mkenya kuhakikisha kuwa wanampa nafasi naibu wa Rais kutenda kazi aliokuwa amechaguliwa kufanya badala ya kumuhukumu haraka kwa kosa ambalo linaweza likatatuliwa kupitia mazungumzo.
Aidha Mugo amewakashifu wabunge kwa kile amesema kuwa wanaubaguzi kwa masuala ya maendeleo kwani wanalipa kipaumbele swala la kumbandua afisini naibu wa rais badala ya kuangazia maswala muhimu kama bima mpya ya Afya SHA, ambayo Wakenya wanahitaji kueleweshwa kwa kina.
Hata hivyo Mugo amewataka viongozi kuasi kuzozana na kuungana ili kupisha maendeleo katika taifa la Kenya.