Mapacha wauliwa Dukana, Marsabit kutokana na Imani kuwa wataletea familia ‘Nuksi’.
January 22, 2025
Vyombo vya habari kaunti ya kaunti ya Marsabit vinafaa kuwa makini na habari vyanavyopeperusha kwenye vituo vyao.
Haya yamekaririwa na Kamishina wa kaunti ya Marsabit Paul Kamau.
Akizungumza kwenye mkutano ya wanahabari na wakuu wa idara mbalimbali ya serikali hii leo, Kamau amesema kuwa kaunti ya Marsabit imejulikana na jina mbaya kwa wengine kutokana na baadhi ya habari ambazo zimekuwa zikipeperushwa huku akiwapongeza wanahabari kwa kuunganisha serikali na wananchi hapa jimboni Marsabit.
Aidha kamishina Kamau amekiri kuwa wawekezaji wengi wanatoka kaunti hii na kuenda kwingine kuwekeza huku akiwataka wanahabari wa Marsabit kuwa mabalozi wema kwa kupeperusha habari zinazolifaa jimbo hili.
Kwa upande wake mratibu wa baraza la vyombo vya habahari MCK ukanda wa mashariki Jackson Karanja ni kuwa wanahabari wanaweza kuchangia maendeleo ya kaunti hii kwa kupeperusha mazuri ya kaunti ya Marsabit