Understanding Elavil: Uses, Benefits, and Safety
December 26, 2024
VIONGOZI waliochaguliwa katika eneobunge la Laisamis kaunti ya Marsabit wametaja safari ya naibu rais Kithure Kindiki siku ya Jumapili kuwa yenye manufaa kwao ikizingatiwa ahadi ambazo Kindiki alizitoa kwa wakaazi hao.
MCA wa Korr/Ngurnit Daud Tomasot akizungumza na radio jangwani ameonesha Imani kuwa ahdi ya kaunti ndogo ya Korr itawafaa sana kwani huduma nyingi za serikali itakuja karibu nao ikizingatiwa kuwa kwa miaka mingi wakaazi wa wadi yake wamekuwa wakisaka huduma za serikali mjini Laisamis hatua wanayosema huwa ni gharama kwao.
Ameongeza kuwa nafasi za ajira sasa zitawafikia kwani ofisi hiyo huja na mengi mazuri kinyume na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Ameongeza kuwa naibu rais wa taifa kufika eneo hilo la mashinani kurejesha shukrani kwa wananchi baada ya kuwapa kura ni hatua kubwa wanayoichukulia kwa heshima kubwa.
Wanatumai kuwa yote walioahidiwa itatimizwa ili kuona umuhimu wa safari hiyo.
Naibu rais prof Kithure Kindiki Jumapili alihudhuria ibada ya kanisa eneo la Korr na kuahidi mengi mazuri ikiwemo kusuluhisha baadhi ya kero kama vile ukosefu wa maji, umeme, usalama kati ya mengine.