Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Vijana wa kaunti ya Marsabit wametoa hisia zao kuhusiana na ukosefu wa ajira.
Baadhi ya waliozungumza na Shajara ya Radio Jangwani, wamelalamikia kuwa ukabila na ufisadi ndio kikwazo kikuu katika upatikanaji wa ajira hapa nchini.
Wamesema kuwa idadi kubwa ya watu wanaajiriwa kwa misingi ya kabila huku wakihisi kutengwa kutokana na mifumo inayotumika kuwaajiri watu ambayo wanataja kwamba haiwatendei haki.
Aidha wameitaka serikali kuingilia kati na kutatua changamoto hizi kwa kuhakikisha kuwa nafasi za ajira zinatolewa kwa njia ya usawa na haki kwa wote.