Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na JB Nateleng & Abdilaziz Abdi,
Vijana katika kaunti ya Marsabit wameshauriwa kuwasaidia wazazi wao kujisajili kwenye bima mpya ya afya ya SHIF.
Kwa Mujibu wa naibu kamishna wa Marsabit ya kati David Saruni ni kuwa vijana wanauwezo wa kusaidia serekali kusajili watu wengi kwa sababu wanauzoefu wa kutumia mitandao na pia simu na kuwataka kuwa kwenye mstari wa mbele kusaidia kuwafikia hata walio mashinani.
Saruni ameelezea hoja ya kujisajili ili kunufaika na bima hii kwani hakuna ada yoyote ya usajili inayotozwa.
DCC Saruni amesema kuwa bima ya SHIF haijaweka idadi kamili ya wale ambao wanapaswa kuongezwa kama watakaonufaika na bima hii maarufu Beneficiaries.
Kauli yake imeungwa mkono na machifu kutoka lokesheni ya Dakabaricha wakisema kuwa wananchi wanapaswa kuenzi bima hii kwani inamanufaa mengi ambayo yatawasaidia katika kupata huduma bora za afya.