Viongozi wa kidini wakemea kisa cha mauaji ya mapacha Dukana, Marsabit
January 24, 2025
Na Isaac Waihenya,
Vijana katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kujiunga na biashara badala ya kutegemea kujiariwa.
Kwa mujibu wa mmoja wa wakurugenzi wa chama cha wafanyibiashara KNCCI Tawi la Marsabit Joseph Gubo ni kuwa vijana wanafaa kuangazia kujiari badala ya kuajiriwa ili kuhakikisha kwamba wanatatua swala la ukosefu wa ajiri hapa nchini.
Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya kipekee, Gubo amesema kuwa vijana wanatalanta ambazo zinazoweza kuwapa ajira na kipato kizuri hata zaidi ya kile cha kuajiriwa.
Aidha Gubo ameitaka serekali kuingilia kati na kutatua swala la bidhaa gushi ambazo zinaadhiri biashara hapa jimboni.
Kauli yake imeungwa mkono na afisa kutoka shirika la serekali chini ya wizara ya vyama vya ushirika Micro-Small Enterprise Authority (MSEA) Simeon Umoro ambaye amewataka vijana kutohofia kuchukua mikopo kujiendeleza kibiashara.