Serikali ya kaunti ya Marsabit yaondolea wazazi wasiwasi kuhusu hatima ya ufadhili wa elimu.
January 21, 2025
Usalama umeimarishwa katika kijiji cha Abbo kaunti ndogo ya Sololo katika kaunti ya Marsabit baada ya zaidi ya wahalifu wapatao 20 wanaoaminika kutoka nchi jirani ya Ethiopia kuvamia kijiji hicho na kuanza kufyatua risasi kabla ya kutoweka kuelekea eneo la Dukale nchini Ethiopia.
Kulingana na kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo ni kuwa hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa katika kisa hicho kilichojiri siku ya jumapili ya tarehe 10 mwezi huu wa Novemba.
Aidha Kamanda Kimanyo ameweka wazi kuwa maafisa wa KDF kwa ushirikiano na maafisa wa vitengo mbalimbali vya polisi wanashika dori katika eneo hilo ili kuimarisha usalama