SERIKALI YASISITIZA KUWA CHANJO YA MIFUGO INALENGA KUPANUA SOKO LA MIFUGO LA KIMATAIFA.
December 18, 2024
Baraza Kuu la Waislamu nchini, SUPKEM tawi la Marsabit, limeonyesha mshikamano wake na Mwenyekiti wao wa kitaifa, Hassan Ole Naado, katika wito wake wa umoja na viongozi wa kanisa kwa lengo la kusukuma serikali kushughulikia masuala muhimu ya umma.
Kupitia kwa Katibu wao, Omar Kutara, baraza hilo limezungumzia umuhimu wa serikali kusikiliza maoni na mapendekezo ya viongozi wa dini na kutekeleza mikakati thabiti ya kuboresha hali ya jamii kwa ujumla.
Wamehimiza serikali kuhakikisha kwamba huduma muhimu kama vile elimu, afya, na usalama wa jamii zinapewa kipaumbele cha juu ili kuleta maendeleo na ustawi kwa wananchi wote.
Baraza hilo linasisitiza umuhimu wa kushirikiana kwa pamoja katika kujenga jamii bora na imara.
Omar, ambaye amesisitiza umuhimu wa kumaliza ufisadi ili kuleta uongozi bora nchini,Amesema kwamba Kenya ina rasilimali nyingi ambazo zinaweza kuleta maendeleo endapo zitatumika ipasavyo.