Understanding Elavil: Uses, Benefits, and Safety
December 26, 2024
Siku moja tu baada ya naibu wa Rais Rigathi Gachagua kumuomba msamaha Rais Wiliam Ruto kuhusiana na iwapo amekosea na kupelekea mswaada wa kutaka abanduliwe mamlakani kufikishwa bungeni, baadhi ya wakaazi wa Marsabit wametoa maoni yao kuhusiana na hatua hiyo.
Baadhi ya waliozungumza na Shajara ya Radio Jangwani wametaja kuwa Gachagua kama binadamu yeyote yule huenda alikosea na anafaa kusamehewa haswa baada ya kuomba msamaha.
Wametaja kwamba kuwa naibu wa rais anafaa kupewa nafasi ili abadilike.
Aidha wengine wao wamehisi kwamba komba msamaha kwa Gachagwa kunashiria kuwa anahusika kwa mashtaka yote yanayo mkabili na hivyo basi kutaka ang’olewe mamlakani.
Wengine wao wametaja kwamba Gachagua anafaa kubanduliwa mamlakani ili Rais Ruto apate upinzani kutokana na upinzani kujiunga na serekali.