Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na JB Nateleng,
Kufuatia agizo la serekali la kuwaruhusu wakenya kutembelea mbuga za Wanyama bila malipo jumamosi hii, shirika la wanyamapori (KWS) Marsabit limewashauri wananchi kuchukua fursa hii na kutembelea mbuga mbalimbali za Wanyama hapa jimboni.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya Kipekee, msimamizi wa Mbuga za wanyama pori katika kaunti ya Marsabit Gilbert Njeru ameelezea kuwa siku hiyo(Jumamosi) mbuga za Wanyama hapa Marsabit zitakuwa wazi kwa kila mmoja hivo kuwarai wananchi jimboni kuchukua fursa hiyo kuweza kutalii mbuga hizo na pia kuweza kujua aina ya Wanyama ambao wanaishi kule.
Gilbert amewataka wakuu wa taasisi na shule kuchukua fursa hii adhimu kuwaleta wanafunzi na wafanyakazi kufurahia mbuga ya Marsabit
Gilbert amewataka wanaMarsabit kujitokeza kwa wingi na kuweza kupata mafunzo ambayo yatawafanya kuenzi mbuga za Wanyama na pia kuelewa vyema kuhusu msitu wa Marsabit ambao ndio kivutio cha watalii hapa jimboni
Japo dunia itasherehekea siku ya utalii hapo kesho Gilbert hata hivyo amesema kuwa, watajiunga na wenzao wa shirika la kuhifadhi misitu(KFS) katika kuzindua Mpango wa usimamizi wa misitu (PFMP) zoezi liitaloongozwa na waziri wa mazingira Adan Duale.