MILA NA TAMADUNI ZATAJWA KUWA KIKWAZO KWA WANAWAKE KUFANYA MAZOEZI YA MWILI MARSABIT.
November 20, 2024
SERIKALI ya kitaifa imetakiwa kushughulikia kwa haraka ukosefu wa chakula na njaa inayokumba wananchi katika sehemu nyingi za kaunti ya Marsabit kutokana na ukosefu wa mvua iliofeli msimu wa upanzi.
Mwakilishi wadi wa Korr/Ngurnit Daud Tomasot ameambia shajara ya radio jangwani kuwa sehemu nyingi za jimbo la Marsabit kwa sasa inashuhudia ukosefu mkubwa wa chakula hivyo kuitaka serikali ya kitaifa kuwapa wananchi wa Marsabit chakula cha msaada.
Kuharibu hali Zaidi, MCA huyo ameishambulia serikali kuu kwa kuchelewa kutoa pesa za mgao wa kaunti mbali mbali nchini suala analotaja kuwa limeathiri maisha ya wafanyakazi wengi wa kaunti ya marsabit ambao kwa sasa anasema wamesalia omba omba.
Wakti uo huo ameondolea lawama serikali ya kaunti na uongozi wake akidai sio wao ndio wanaochelewesha mishahara yao bali ni mgao wa kaunti ndio haujatumwa.
Kuhusiana na sera ambazo si maarufu katika serikali ya sasa Tomasot amesema kuwa wanaochangia pakubwa matatizo hayo ni wabunge na maseneta kwani wao ndio wanaopitisha na kuidhinisha sheria bungeni.