Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Caroline Waforo,
Raia wawili wa Ethiopia na mkenya moja wameshtakiwa katika mahakama ya Marsabit kwa mashtaka kadhaa ikiwemo kumiliki silaha haramu.
Washukiwa hao ambao wanajumuisha mkenya Roba Sora almaarufu Kolo, raia wa Ethiopia Rob Jarso almaarufu Salo pamoja na Galgallo Boro almaarufu Halkano walikamatwa tarehe 15 mwezi Oktoba mwaka 2022 katika Manyatta ya Goro Rukesa lokesheni ya Qilta Korma katika eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit na kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tarehe 31 mwezi Oktoba mwaka wa 2022 mbele ya hakimu mwandamizi Simon Arome.
Mshukiwa wa kwanza mkenya Roba Sora alishtakiwa kwa makossa mawili. Kosa la kwanza ni kumiliki silaha haramu baada yake kukamatwa na bunduki moja aina ya AK47, kosa la pili ni kumiliki risasi 13 kinyume cha sheria.
Nao raia hao wawili wa Ethiopia wameshatakiwa kwa makosa matatu. Kosa la kwanza ni kumiliki silaha haramu baada yao kukamatwa na bunduki aina ya SHE Rifle bila leseni. Kosa la pili likiwa ni kumiliki risasi 13 kinyume cha sheria na kosa la tatu likiwa ni kuwa hapa nchini kinyume cha sheria.
Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena tarehe 9 mwezi Oktoba 2024.