Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Raia saba wa Ethiopia wameshtakiwa katika mahakama ya Marsabit kwa kosa la kuwa nchini Kenya kinyume na sheria.
Mahakama imearifiwa kuwa mnamo tarehe 2 mwezi huu wa Octoba, katika daraja la Laisamis lililoko katika barabara kuu ya Isiolo-Marsabit kaunti ya Marsabit raia hao saba wa Ethiopia walikamatwa wakiwa nchini bila stakabathi hitajika.
Walikuwa wakisafiri kutumia gari aina ya Toyota Land Cruiser yenye nambari ya usajili KBB 263G.
Saba hao walifikishwa mahakamani tarehe 3 mwezi huu wa Octoba mbele ya hakimu mwandamizi Simon Arome ambapo walikubali kosa dhidi yao.
Walidai kuwa maisha yao yamo hatarini nchini Ethiopia na kuomba hifadhi humu nchini Kenya.
Hakimu mwandamizi Simon Arome aliitaka idara ya wakimbizi kuwahoji saba hao.
Gari walimokuwa wakisafiria limetwaliwa na serikali.
Raia hao wa Ethiopia wataendelea kuzuiliwa huku kesi hiyo ikiratibiwa kutajwa tena tarehe 21 mwezi huu wa Octoba.