Serikali ya kaunti ya Marsabit yaondolea wazazi wasiwasi kuhusu hatima ya ufadhili wa elimu.
January 21, 2025
Polisi katika kaunti ya Isiolo wamefanikiwa kunasa zaidi ya kilo 200 za bangi katika eneo la Kambi Samaki kaunti ndogo ya Garbatulla.
Akidhibitisha kisa hicho Kamanda wa polisi kaunti ya Isiolo Moses Mutisya amesema bhangi hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 6 ilikuwa ikisafirishwa kuelekea Garissa.
Washukiwa walifanikiwa kutoroka.
Kamanda Mutisya ametoa onyo kali kwa walanguzi wa mihadarati na pamoja na pombe haramu akidokeza kuwa sheria itachukua mkondo wake.
Kadhalika amepoongeza vikosi vya usalama Isiolo kwa kuzuia bhangi hiyo kuingia sokoni na kuwa tishio kwa wanafunzi ambao wako likizoni
Anasema hilo limewefanikshwa na operesheni inayoendeshwa na asasi za usalama