Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Polisi katika kaunti ya Marsabit wamemuua mhalifu mmoja katika eneo Badasa baada ya jaribio la wizi wa mifugo kutibuka.
Akithibitisha kisa hicho kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Marsabit ya kati, Edward Ndirangu amesema kuwa kisa hichi kilijiri jana saa sita mchana, ambapo watu waliokuwa wamejihami na bunduki walivamia wafugaji katika eneo la maji la Ell Nedeni na kujaribu kuiba mbuzi zaidi ya 100 ambao waliweza kurejeshwa na maafisa wa polisi waliofika katika eneo hilo.
Ndirangu amsema kuwa katika kisa hicho cha jaribio la wizi wahalifu waliweza kuwapiga watu wawili risasi.
Wawili hao walipata majeruhu madogo na walipekwa katika hospitali ya rufaa ya Marsabit ambapo walipokea matibabu.
Hata hivyo Ndirangu amefichua kuwa waliotekeleza uvamizi huo ni majambazi kutoka kaunti jirani huku akiwarai wananchi kutoa kuripoti zozote kuhusiana na uhalifu ili kuhakikisha kwamba usalama unadumishwa kikamilifu.