Wanawake wawili wanaendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Moyale baada ya kunaswa na vidonge 25 vya cocaine zenye thamani ya shilingi milioni 1.2 katika kituo cha mabasi cha Moyale kaunti ya Marsabit hapo jana Jumatano.
Hii ni bada ya wawili hao kufikishwa katika mahakama ya Moyale leo hii ambapo upande wa mashataka uliomba siku 14 kufanya uchuguzi wake.
Kulingana na kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo jana jumatano, mida ya saa tano asubuhi, wanawake hao walinaswa katika kituo cha mabasi mjini moyale wakisafirisha cocaine hiyo iliyokuwa imefichwa ndani ya nguo zao za ndani.
Kamanda Kimaiyo amethibitisha kuwa bangi hiyo ilikuwa inasafirishwa kutoka nchi jirani ya Ethiopia kwani wawili hao walikuwa na risiti za gari zilizoashiria kuwa walikuwa wanatoka jijini Adis Ababa, Ethiopia.
L