Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Mwenyekiti wa shirikisho la mpira wa miguu FKF tawi la Marsabit Mohamed Nane amekanusha madai kuwa amejiuzulu na kujiondoa katika kinyanganyiro cha mweyekiti wa shirikisho hilo kwenye uchaguzi mkuu wa Disemba 11 mwaka huu.
Akizungumza na Radio Jangwnai kwa njia ya simu, Mohamed Nane ameutaja uvumi huo kama propaganda zinzoenezwa na wapinzani wake.
Nane ametaja kwamba bado hakina mabadiliko katika timu ambazo zitaruhusiwa kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Nane amewashtumu wawakilishi wadi kwa kile amekitaja kwamba ni kutowajibika kazini mwao kuhakikisha kwamba fedha zinazotengewa idara ya michezo hazitumiki vibaya wala kutomiwa katika idara zingine.
Aidha Nane amependekeza mageuzi katika idara ya michezo kaunti ya Marsabit huku akitaja kwamba hilo ndilo litakalo saidia kuhakikisha kwamba idara hiyo inapiga hatua.