Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Caroline Waforo,
Mwanaume moja ameshtakiwa katika mahakama ya Marsabit kwa kosa la wizi wa kimabavu.
Mahakama ya Marsabit imearifiwa kuwa mnamo tarehe 25 mwezi machi mwaka 2024 katika Kijiji cha Mata Arba lokesheni ya Dakabaricha kaunti ya Marsabit mshukiwa kwa jina Abdub Guracha Guyo kwa ushirikiano na watu wengine waliojihami kwa bunduki walimvamia mwanaume moja kwa jina George Guyo Umme na kumwibia kitita cha shilingi 320,000.
Mtuhumiwa alikamatwa tarehe 26 mwezi machi 2024 na kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mbele ya hakimu mwandamizi Simon Arome tarehe 28 mwezi machi mwaka huu.
Aidha Tarehe 14 mwezi Mei mwaka huu mtuhumiwa alipewa bondi ya shilingi 1,000,000 aliyoshindwa kulipa.
Anaendelea kuzuiliwa huku kesi ikiendelea.
Kesi hii itatajwa tena terehe 15 mwezi ujao wa Octoba.