County Updates, Diocese of Marsabit, Editorial, Local Bulletins, National News

MWANAMKE MMOJA AJITIA KITANZI NYUMBANI KWAO KATIKA KIJIJI CHA MANYATTA SHRINE, ENEO BUNGE LA SAKU, KAUNTI YA MARSABIT

Na JB Nateleng & Naima Abdullahi

Mwanamke mmoja mwenye umri wa makamu amejitia kitanzi nyumbani kwao katika kijiji cha Manyatta shrine, eneo bunge la Saku, kaunti ya Marsabit

Akithibitisha kisa hicho Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Marsabit ya kati, Edward Ndirangu amesema kuwa kisa hichi kilijiri Jana saa mbili usiku, ambapo mwendazake alijinyonga kwa kutumia kitanbaa cha nguo.

Mwili wa mwendazake ulipatikana majira ya jioni ukininginia juu,huku akiwa amejifunga nguo shingoni yake.

Kulingana na Kamanda Ndirangu ni kuwa kilichopelekea kitendo hicho bado haikubainika,huku maafisa wa usalama wakiendelea na uchunguzi ili kubaini kilichopelekea mwanamke huyo kujitoa uhai.

Mwili wa mwendazake umehifadhiwa katika makafani ya hospitali ya rufaa ya Marsabit.

Subscribe to eNewsletter