Viongozi wa kidini wakemea kisa cha mauaji ya mapacha Dukana, Marsabit
January 24, 2025
Wazazi wa msichana moja mwenye umri wa miaka 16 wamehukumiwa kufungo cha miaka mitatu gerezani kwa makosa manne yanayofungamana na kumwoza msichana huyo katika kaunti ya Marsabit.
Inaarifiwa kuwa kati ya tarehe 30 mwezi Agosti na tarehe 3 mwezi Septemba mwaka 2023 katika kijiji cha Lokileleng’i kaunti ya Marsabit watuhumiwa Aluano Bursuna na Jalaa Bursuna walimuoza mwanao wa miaka 16 kwa mzee Alois Leparkeri.
Wawili hao walikamatwa tarehe 4 mwezi September 2023 na kufikishwa katika mahakama ya Marsabit mbele ya hakimu mwandamizi Christine Wekesa kwa mara ya kwanza tarehe 6 mwezi September mwaka uo huo.
Makosa hayo manne yanajumuisha kumwoza msichana huyo, kuruhusu akeketwe, kuruhusu makazi yao kutumika kuendesha zoezi la ukeketaji pamoja na kufeli kuripoti kisa cha mwanao kukeketwa kwa maafisa husika.
Wakati wa kesi hiyo ilibainika kuwa msichana huyo alikeketwa tarehe 8 mwezi wa agosti siku mbili baada ya kufunga shule kwa likizo ya muhula wa nane.
Aidha ilibainika kuwa siku mbili baada ya kukeketwa mwanaume aliyeozwa kwake kwa jina Aloise Leparkeri alimtembelea nyumbani kwao na kumnajisi. Kitendo ambacho Aloise aliendelea kukitekeleza kati ya tarehe 10 hadi 13 mwezi huo wa Agosti kabla ya msichana huyo kupokezwa kwake tarehe 30 mwezi uo huo.
Kesi hiyo ilisikilizwa tarehe 16 mwezi huu wa Septemba huku Aluano Bursuna ambaye ni mamake mwathiriwa akipatikana na hatia katika makosa yote manne na kupigwa faini ya shilingi 200,000 au kifungo cha miaka 3 gerezani kwa kila kosa kifungo na ambacho kutatekelezwa kwa wakati moja.
Hii ikimaanisha kuwa atatoa faini ya shilingi 800,000.
Naye Jalaa Bursuna babake msichana huyo alipigwa faini ya shilingi 200,000 au kifungo cha miaka 3 gerezani kwa kosa la kwanza.
Wawili hao wana siku 14 kukata rufaa.