MILA NA TAMADUNI ZATAJWA KUWA KIKWAZO KWA WANAWAKE KUFANYA MAZOEZI YA MWILI MARSABIT.
November 20, 2024
Mtihani ya kitaifa ya gredi ya sita KPSEA umeongo’a nanga rasmi hii leo huku wanafunzi wakikalia mtihani wa Hesabu na kingereza.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri ni kuwa ni jumla ya watahiniwa 8,383 wa shule za msingi ambao wamekalia mtihani huo katika vituo vya mitihani 210.
Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya simu, Magiri ametaja kwamba idadi ya wavulana wanao kalia mtihani huo ni 4,219 huku wasichana wakiwa ni 4,164.
Mkurugenzi huyo wa elimu ametaja kwamba japo kuna visa vichache vya wanafunzi kukosekana hii leo ikiwa ndio siku ya kwanza ya mtihani huo, ila idadi kubwa ya wanafunzi wamefanya ya kwanza miwili.