October 30, 2024
MITIHANI YA KITAIFA KPSEA WAKAMILIKA HII LEO, WANAFUNZI 8,383 WAKIKALIA MTIHANI HUO KAUNTI YA MARSABIT.
Mtihani ya kitaifa ya gredi ya sita KPSEA 2024, umekamilika rasmi hii leo huku wanafunzi wakikalia mtihani wa mwisho wa Creative Art and Social Studies.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri ni kuwa ni jumla ya watahiniwa 8,383 wa shule za msingi ambao wamekalia mtihani huo katika vituo vya mitihani 210.
Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya simu, Magiri ametaja kwamba idadi ya wavulana wanao kalia mtihani huo ni 4,219 huku wasichana wakiwa ni 4,164.
Mkurugenzi huyo wa elimu ametaja kwamba japo kuna visa vichache vya wanafunzi kukosekana, ila idadi kubwa ya wanafunzi wamefanya mtihani huo wa kitaifa.
Magiri amesifia namna baraza la mitihani nchini KNEC lilijiandaa kuhakikisha kwamba mtihani huo unafanyika kwa njia bora.