Mtu mmoja afariki kutokana na ugonjwa wa Kalazaar Marsabit, sita wakipokea matibabu kulingana na serikali ya kaunti.
February 21, 2025
Huku mtihani wa kitaifa ya KCSE ukiingia wiki yake ya pili hii leo,mkurugenzi wa elimu kaunti ya Marsabit Peter Magiri amesema kwamba zoezi hilo limekuwa likiendelea vyama kama ilivyoratibiwa.
Akizungmza na Shajara ya Radio Jangwani afisini mwake, Magiri amesema kuwa licha ya mvua chache ambazo zimeshuhudiwa katika maeneo kadhaa hapa jimboni, mitihani hiyo imeendelea vyema katika wiki yake ya kwanza.
Aidha Magiri amewasifia wasimamizi wa mtihani huo kwa kuhakikisha kuwa hakujakuwa na visa yoyote vya udanganyifu.
Hata hivyo mkurugenzi huyo wa elimu amewarai wanafunzi kutokuwa na fikra za udanganyifu kwa mtihani uanoendelea mbali wajitahidi ili wapate matokeo yanayofaa.