Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Idadi kubwa ya watahiniwa huria maarufu Private Candidates katika kaunti ya Marsabit kwenye mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE mwaka huu imechangiwa na matokea bora ya watahiwa huria 48 waliokalia mtihani huo mwaka jana.
Kwa mujibu wa washikadau katika idara ya elimu kaunti ya Marsabit ni kuwa watahiniwa huria 48 waliokalia mtihani huo mwaka jana walifaulu kwa kupata alama ya C Plain kwenda juu jambo lililochochea wengine kujiunga na masomo na kujisajili kwa mtihani wa KCSE mwaka huu.
Kwenye mtihani wa KCSE mwaka huu jumla ya wanafunzi huria 157 watakalia mtihani huo katika kauti ya Marsabit, 76 wakiwa ni wakike huku 81 wakiwa ni wakiume.
Kwenye mkao na meza ya habari ya Radio Jangwani, washikadau hao wametaja kwamba idadi hiyo ni ya juu zaidi ikilinganishwa na miaka ya hapo nyuma.
Wameweka wazi kuwa watahiniwa wamejiandaa kikamilfu sawa na wezao wengine kutoka shule mbalimbali za upili hapa jimboni Marsabit.