Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Madereva wawili wameshtakiwa katika mahakama ya Marsabit kwa kosa la kuwasafirisha raia 24 wa Eritrea humu nchini kenya kinyume na sheria.
Mahakama imearifiwa kuwa mnamo tarehe 6 mwezi huu wa Octoba katika eneo la kibiashara la Turbi lililoko katika barabara ya Turbi kuelekea Forole, kaunti ndogo ya Turbi kaunti ya Marsabit washukiwa Ali Abdikadir Ali na Gara Diba Ibrae walikamatwa wakiwasafirisha raia 24 wa Eritrea kutumia gari aina Toyota Voxy yenye nambari ya usajili KDE 316F kinyume cha sheria.
Wawili hao wamefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Jumatatu 7 Oktoba, mbele ya hakimu Mwandamizi Simon Arome ambapo wamekana mashtaka dhidi yao.
Wameachiliwa kwa bondi ya shilingi 500,000 au pesa taslimu 500,000.
Kesi hiyo itatajwa tena terehe 14 mwezi huu wa Octoba.