Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Wito wa amani umeendelea kutolewa kwa wakaazi jimboni Marsabit.
Wakizungumza hapo jana wakati wa sherehe ya siku kuu ya Mashujaa iliyoandaliwa katika eneo la Kubi Dibayu wadi ya Sagante Jaldesa eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit, baadhi ya wazee wanachama wa kamati ya usalama waliwapongeza wakaazi jimboni kwa kuiitikia wito wa kuishi kwa amani na utangamano.
Naibu mwenyekiti wa kamati hiyo Adan Chukulisa amewaeeleza wakaazi kwamba amani ndio msingi wa maendeleo katika jamii.
Kwa upande wake Fred Lekesike ambaye ni mwanachama wa kamati hiyo ameeleza kuwa wanawashirikisha vijana katika juhudi za kuendelea kutafuta amani jimboni Marsabit.
Naye chifu wa Kamboe Samuel Kapina amewaomba wakaazi kuendelea kudumisha amani.
Watatu hao ni baadhi ya watu 11 waliotuzwa kwa juhudi zao za kuleta amani jimboni baada ya kipindi kirefu cha mizozo ya kijamii.
5 walituzwa hapo jana huku 6 wakituzwa mwezi Septemba wakati wa maadhimisho ya siku ya amani ulimwenguni.