MILA NA TAMADUNI ZATAJWA KUWA KIKWAZO KWA WANAWAKE KUFANYA MAZOEZI YA MWILI MARSABIT.
November 20, 2024
Mabadiliko ya tabia nchi huathiri pakubwa kinamama wanaoishi mashinani na kuwafanya wengine kuyahama makazi yao ili kutafata ajira mjini.
Haya ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa shirikia la Wong`an Women Initiative Teresalba Leparsanti
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, Teresalba amesema kuwa kinamama wanaoishi mashinani huwa wanaathirika pakuwa wakati wa ukame kwa sababu waume wao wanapofuata mifugo kutafta malisho wanasalia wakitaabika wasijue chha kufanya.
Kutokana na hilo inawabidi wengine kuhamia mjini kutafta ajira ambayo pia kwa kiwango kikubwa wanakandamizwa kwa kupewa malipo duni ambayo haimudu kusaidia familia zao.
Teresalba ameelezea kuwa kinamama hao kwa mara nyingi wanapitwa na mengi mojawepo ikiwa elimu ya ujuzi mashinani ili kujitafutia mapato tofauti na wenzao walioko katika maeneo ya miji.
Teresalba ametoa wito kwa serekali pamoja na mashirika yasiyo ya kiserekali kutoa mafunzo kwa kina mama hao walioko mashinani ili kuwapa fursa ya kujitegemea wenyewe.