Afueni kwa wanafunzi 132 wa shule ya upili ya Goro Rukesa baada ya KNEC kuachilia matokeo ya mitihani yao….
January 21, 2025
Kituo cha kuwalinda na kuwahifadhi waadhiriwa wa dhulma za kijinsia katika eneo la Loglogo (Loglogo Rescue Center) kaunti ya Marsabit kitafunguliwa januari mwaka ujao wa 2025.
Haya ni kwa mujibu wa afisa wa jinsia katika kaunti ya Marsabit Joshua Akeno Leitoro.
Akizungumza na Radio Jangwani baada ya kukamilika kwa warsha ya siku tatu ya kuangazia namna ya kufufua kituo hicho Leitoro ametaja kwamba mikakati kambambe imewekwa kuhakikisha kwamba kituo hicho kinafanya kazi ili kuwalinda waadhiriwa wa dhulma za kijinsia.
Aidha Leitoro amezitaja mila potovu kama chanzo kikuu kinachopelekea idadi ya visa vya dhulma za kijinsia kuongezeka hapa jimboni Marsabit huku akitoa wito wa jamii kukomesha mila hizo.
Kadhalika afisa huyu wa jinsia amewarai wazazi kuwalinda watoto kipindi hichi cha likizo kwani dhulma nyingi za kijinsia hutekelezwa msimu wa likizo.
Kwa upande wake mshirikishi wa shirika la Gender Violence Recovery Centre (GVRC), Dolphine Mwango ni kuwa zoezi hili la Kufufua vituo vya kuwalinda na kuwahifadhi waadhiriwa wa dhulma za kijinsia linalenga kaunti 13 ikiwemo Marsabit,kaunti ambazo kiwango cha visa vya dhulma za kijinsia kimetajwa kuongezeka.
Sasa ni afueni baada ya kubainika kuwa kituo cha kuwalinda na kuwahifadhi waadhiriwa wa dhulma za kijinsia katika eneo la Loglogo (Loglogo Rescue Center) kitafunguliwa januari mwaka ujao wa 2025.
Na kama anavyotuarifu mwandishi wetu Isaac Waihenya, kituo hicho kinalenga kuwalinda waadhiriwa wa dhulma za kijinsia katika kaunti ya Marsabit.