Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
UCHIMBAJI wa migodi katika eneo la Hillo eneobunge la Moyale utasalia kufungwa na kuingia eneo hilo kwa saasa ni kinyume cha sheria.
Onyo hilo limekaririwa na Collins Ochieng ambaye ni mwanajiolojia katika kaunti ya Marsabit.
Akizungumza na idhaa hii ofisini mwake Ochieng amesema kuwa ikiwa mgodi huo ungekuwa unafanya kazi idara ya madini katika kaunti ya Marsabit ungetoa mafunzo kwa yeyote Yule ambaye angependa kufanya kazi hiyo na washikadau mbalimbali ambao wanahusika na migodi hiyo.
Kwa sasa anasema kuwa mafunzo hayo hayaenedelei kutokana na kufungwa kwa migodi hiyo ya dhahabu.
Hata hivyo Ochieng amesema kuwa idara ya uchimbaji madini hutoa usajili kwa vyama vya ushirika sio kwa mtu binafsi akisema kuwa kupitia usajili wa vyama migodi hiyo itaweza kuhalalishwa na watu waendelee kunufaika.