KITUO CHA KUOKOA WANAOPITIA DHULMA ZA KIJINSIA KUANZISHWA LOGLOGO KAUNTI YA MARSABIT
November 6, 2024
Itakuwa ni afueni kwa waathiriwa wa dhulma za kijinsia jimboni Marsabit iwapo kituo cha uokoaji katika eneo la Log logo itafunguliwa.
Kwa mujibu wa mwekahazina wa kundi la Isogargaro Women Group Hellen Ildhani ni kuwa kituo hicho kitasaidia katika kuwalinda watoto, pamoja na watu wazima ambao wanapitia dhulma za kijinsia, kwa sababu watapata mahali salama ambapo watahifadhiwa mbali na kunakotokea dhulma.
Hellen amesema kuwa hatua hii pia itasaidia katika kuwafanya waadhiriwa waweze kurejea hali yao ya kawaida na kuishi na watu bila kuwa na moyo wakulipiza kisasi.
Ameitaka wazazi kushirikiana na serekali msimu huu wa likizo ili kudhibiti muziki wa usiku kutokana na madai kuwa huku ndiko vijana wengi hupitia dhulma za kijinsia na pia kujifunza matumizi ya mihadarati..
Hellen amesema kuwa ni sharti jamii iweze kusimama kidete na kuhakikisha kuwa wamepiga marufuku ukeketaji wa Watoto wasichana.
Catherine Ntingiyan Lekuton ambaye ni moja wa waathiriwa wa dhulma za kijinsia amesema ni sharti jamii isimame kidete katika kuhakikisha kuwa wamelinda haki ya wasichana na kuwapa nguvu ya kuendelea mbele.