Serikali ya kaunti ya Marsabit yaondolea wazazi wasiwasi kuhusu hatima ya ufadhili wa elimu.
January 21, 2025
Idara ya afya katika ugatuzi ya Marsabit pamoja na nchi jirani ya Ethiopia imeshirikiana kupiga vita magonjwa ya kupooza na ukambi.
Licha ya Kenya kupiga teke magonjwa hayo miaka mingi iliyopita inadaiwa kuwa magonjwa hayo yanasababishwa na mwingiliano wa karibu na watu kutoka nchi jirani ya Ethiopia.
Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani Qabale Duba ambaye ni mratibu wa ufuatiliaji wa magonjwa katika hospitali ya rufaa ya Marsabit amesema changamoto kubwa ambayo inayowakumba ni upana wa mpaka ya kaunti ya Marsabit na ushirikiano wa karibu kati ya wakaazi za nchi hizi mbili.
Duba aidha amesema ugonjwa wa kupooza au polio imepatikana Ethiopia hivi karibuni hivyo basi serikali ya Kenya na Ethiopia imekubali kushirikiana kufanya kampeni ya chanjo ya ugonjwa huo wa kupooza na kampeni hiyo itaanza katika kaunti ya Marsabit tarehe 28 mwezi huu wa 11.