ULIMWENGU WAADHIMISHA SIKU YA WALEMAVU JANA,HUKU WITO WA KUWAPELEKA WATOTO WALEMAVU SHULENI UKISHEHENI…
December 4, 2024
Serekali ya kaunti ya Marsabit inalenga kuhakikisha kwamba sheria ya kuwalinda walemavu imebuniwa kufikia mwishoni mwa mwaka ujao wa 2025.
Haya yamewekwa wazi na waziri wa idara ya jinsia na utamaduni katika kaunti ya Marsabit Jeremiah Ledanyi.
Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha siku ya walemavu ulimwenguni hii leo iliyandaliwa katika ukumbi wa kanisa Katoliki hapa mjini Marsabit, waziri Ledanyi ametaja kwamba sheria hiyo itahakikisha kwamba walemavu wanapata haki sawa kama ilivyo kwa watu wengine.
Aidha Ledanyi amesema kuwa serekali ya kaunti itahakikisha kwamba ofisi za umaa zina mbinu ya kuwawezesaha watu wanaoishi na ulemavu kupata huduma.
Kadhalika waziri Ledanyi ameyataka mashirika yasiyo ya kiserekali katika kaunti ya Marsabit kuhakikisha kwamba yanawapa nafasi za ajira watu wanaoishi na ulemavu.
Kwa upande wake naibu gavana wa kaunti ya Marsabit Solomon Gubo Riwe amewataka watu wanaoishi na ulemavu kujikubali na kujitokeza kujisajili ili kufaidika na miradi mbalimbali ya serekali.
Vilevile Guba amewata watu wanaoishi na ulemavu kuungana ili waweze kuhusisishwa katika mipango ya serekali.
Kando na hilo Gubo amewataka watu wanaoishi na ulemavu kujitokeza katika vikao vya umaa vya kutoa maoni ili kupendekeza pia miradi ya maendeleo hapa jimboni.
Aidha baadhi ya watu wanaoishi na ulemavu waliohudhuria hafla hiyo wamepogeza hatua zilizopigwa katika kuinua maisha ya walemavu kaunti ya Marsabit huku wakitaka kuhusihswa kwenye mipangilio ya serekali.