Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na JB Nateleng,
Kama njia mojawepo ya kuzuia ajali katika ziwa Turkana, idara ya uvuvi imewatahadharisha wakazi jimboni kuacha kutumia usafiri wa majini kwa sasa kutokana na kuwepo kwa mawimbi na kupanda kwa maji ya ziwa Turkana.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, Sostine Nanjali ambaye ni afisa kutoka idara ya uvuvi kaunti ya Marsabit amesema kuwa, kufikia sasa ni hatari kwa wakazi katika eneo hilo kutumia mashua ambayo haijakagulika na maafisa wa uvuvi ambao wamekita kambi katika eneo hilo kwa sababu, kujaa kwa ziwa Turkana huenda kukasomba pia mashua.
Sostine ameelezea kuwa ni sharti wakazi watilie maanani agizo hili ili kuepuka kupata ajali ziwani.
Amesema kuwa bado wanaendelea kushirikisha jamii ili kubaini sehemu salama ziinazoweza kumudu mradi ambao serekali inadhamiria kuwekeza katika eneo hilo hivi karibuni.
Kuhusiana na Galla la kuhifadhi samaki katika eneo la Loiyangalani ambalo limesombwa na maji, Sostine amedai kuwa kuna mpango wa kusaidia kitengo cha usimamizi wa fukwe (BMUS) pamoja na Co-operative kujenga galla jingine ambalo litasaidia katika kuhifadhi samaki kabla ya kupata suluhisho la kudumu.
Idara ya uvuvi jimboni Marsabit bado inaendelea na ukaguzi wa BMUs na maeneo ambayo yameathirika kwa madhumuni ya kuboresha sekta ya uvuvi ambayo ndio kitega uchumi cha wakazi wanaoishi karibu na ziwa hilo.