Mtu mmoja afariki kutokana na ugonjwa wa Kalazaar Marsabit, sita wakipokea matibabu kulingana na serikali ya kaunti.
February 21, 2025
Idara ya usalama inashirikiana na idara ya elimu katika eneo la Loiyangalani ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wamefanya mitihani yao ya kitaifa bila tatizo lolote.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu naibu kamishna wa eneo la Loiyangalani Stanley Kimanga amesema kuwa kwa ushirikiano na wakazi pamoja na idara ya elimu katika eneo hilo wameweza kubuni mikakati ambayo itahakikisha kuwa usalama wa wanafunzi umedumisshwa.
Kimanga amewataka wakazi wa Loiyangalani kutokuwa na hofu kuhusu usalama wa wanao shuleni akisema kuwa idara ya usalama iko tayari kupambana na tukio lolote ambalo litaathiri usalama.
Kuhusiana na shule ya msingi ya El-molo Bay ambayo imeathiriwa na kujaa kwa ziwa Turkana, Kimanga amesema kuwa wanafunzi ambao wanasoma katika shule hiyo watafanyia mtihani wao wa KAPSEA katika shule hiyo akisema kuwa kufikia sasa viwango vya maji vimepungua.