Levaquin: Comprehensive Guide on Usage, Benefits, and Safety
December 20, 2024
Katika juhudi za kuimarisha usalama jimboni Marsabit idara ya usalama imeanza mchakato wa kuwapiga msasa watu watakaojiunga na maafisa wa akiba NPR.
Akizungumza na shajara ya radio Jangwani kamanda wa Kaunti hii ya Marsabit Leonard Kimaiyo amesema kuwa maeneo yaliyo mipakani yatapewa kipaumbele kutokana na utovu wa usalama ambao umekuwa ukishuhudiwa ikiwemo mashambulizi ya wizi wa mifugo.
Aidha maeneo mengine yaliyo na utovu wa usalama humu jimboni yatapewa kipaumbele.
Shughuli ya kuwapiga msasa wanaojiunga na maafisa hao inaendeshwa na OCPD wa kaunti ndongo jimboni kwa ushirikiano na machifu.
Aidha Kamanda Kimaiyo amewataka wakaazi jimboni Marsabit kuendelea kudumisha amani huku akiwataka kutoa taarifa muhimu Kwa idara za usalama.