Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na JB Nateleng & Isaac Waihenya
Idara ya elimu katika kaunti ya Marsabit imesema kuwa shule msingi ya El Molo bay iliyo katika wadi ya Loiyangalani kaunti ya Marsabit itahamishwa hivi karibuni.
Haya ni kulingana na mkrugenzi wa elimu jimboni Marsabit Peter Magiri.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, Magiri ameelezea kuwa jamii ya Loiyangali imetoa ardhi ambapo shule hiyo pamoja na wakazi wanaweza kuhamia mbali na ziwa Turkana.
Magiri ameirai serekali ya kaunti, pamoja na serekali kuu kwa ushirikiano na mashirika yasiyo ya kiserekali kusaidia katika kuhakikisha kuwa shule hiyo imeweza kuhamishwa na kujengwa upya.
Na huku mtihani wa KAPSEA ikitarajiwa kuanza mwezi ujao mkuu huyo wa elimu jimboni amesema kuwa idara yake itahakikisha kuwa wanafunzi wa shule hizo wanakalia mtihani huo.