Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Licha ya kaunti ya Marsabit kuwa na idadi kubwa ya mifugo imebainika kuwa idadi hiyo haiwezi ikafikia kiwango cha kuuzwa katika soko la kimataifa.
Mkurugenzi wa idara ya mifugo kaunti ya Marsabit Moses Lengarite amesema kuwa soko la kimataifa ni kubwa hivyo taifa la Kenya haliwezi kutosheleza hilo kutokana na baadhi ya vikwazo ikiwemo kutokuwepo kwa idadi toshelezi ya mifugo, magonjwa ya mifugo katika ya nyingine.
Ili soko la mifugo nje ya Kenya liwepo, anasema ni sharti idadi ya mifugo toshelezi iwe kila mara.
Aidha amesema Marsabit kupakana na taifa la Ethiopia inamaanisha soko kuu la kununua mifugo ni taifa hilo suala linalohatarisha kutokana na magonjwa ya mifugo.
Pia anasema hilo kufaulu lazima pawepo na kituo cha kuzalisha mbegu ya mifugo ili kuendana na mifugo inayokua kuambatana na eneo flani.