WAKAAZI WA MARSABIT WAONESHA MATUMAINI YA KESI ZAO KUKAMILISHWA HARAKA NA MFUMO WA AJS
November 22, 2024
Na Isaac Waihenya,
Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya Kimataifa ya Lugha ya Ishara maarufu International Sign Language Day, wito umetolewa kwa jamii ya Marsabit kutowaficha watu wanaoishi na ulemavu.
Kwa mujibu wa ACC wa Marsabit Andrew Chepkonga ni kuwa jamii imekuwa ikiwaficha watu wanaoishi na ulemavu na kuwanyima haki zao za kimsingi.
Akizungumza hii leo katika shule ya msingi ya SKM hapa mjini Marsabit katika sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya lugha ya ishara,Chepkonga amewataka wananchi wa Marsabit kuhakikisha kwamba watu wanaoishi na ulemavu wanapata haki zao za kimsingi kama ilivyo kwa watu wengine.
Kauli yake iliungwa mkono na afisa wa elimu anayeshugulikia wanafunzi wanaoishi na ulemavu katika eneo bunge la Saku, Dakii Jaldesa amabaye ametaja kuwa jamii inafaa kuasi kasumba ya kuwatelekeza watoto wanaoishi na ulemavu na kuhakikisha kuwa wanapelekwa shuleni kupata elimu.
Hata hivyo mwalimu wa ishara katika shule ya msingi ya SKM Samoea Jacob amekariri hoja ya wanafunzi wanaoishi na ulemavu kupewa elimu kwani pia wanauwezo kama wanafunzi wengine.
Kadhalika mwakilishi wa watu wanaoishi na ulemavu hapa mjini Marsabit Churko Gobe maarufu Alfa Mchoraji ametaja kuwa ipo hoja serekali kuwekeza katika kuwainua watu wanaoishi na ulemavu kwa kuhakikisha kwamba wanawakilishwa katika nafasi mbalimbali serekalini.