Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Huku ulimwengu ukiadhimisha mwezi wa kutoa hamasa kuhusiana na saratani ya matiti duniani wito umetolewa kwa akinamama kujitokeza kufanyiwa ukaguzi kuhusiana na ugonjwa huo.
Kwa mujibu ya muunguzi kwenye kituo cha saratani katika hospitali ya rufaa ya Marsabit, Joyce Mokuro asilimia 16.2 ya watu hapa nchini wameadhirika na ugonjwa huo.
Akizungumza na Shajara na Radio Jangwani ofisi mwake Mokuro amesema kuwa saratani ya matiti ni mojawapo ya magonjwa ya saratani ambayo inapelekea idadi kubwa ya maafaa kwa akinamama.
Aidha Mokuro ametaja kuwa ugonjwa huo unasababishwa na umri,vyakula au hata mtu anaweza akauridhi kutoka wanafamailia.
Kadhalika Mokuro amesisitiza hoja ya akinamama Kufanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara na kuanza matibabu mara moja iwapo watapatikana na maradhi hayo.