Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Idadi ya vijana wanaoambukizwa virusi vya Ukimwi kaunti ya Marsabit inazidi kuongezeka.
Haya ni kwa mujibu wa mtetezi wa watu wanaoishii na virusi vya ukimwi jimboni Marsabit Mwalimu Qabale Tache.
Akizungmza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee, Qabale amesema kuwa hali hiyo imechangiwa na ukosefu wa hamsa haswa kwa vijana kuhusina na virusi vya Ukumwi na namna ya kuzuia kuambukizwa.
Hata hivyo Qabale amewarai vijana kujitokeza kwa kupima hali yao ya HIV kabla ya kujihusisha kwenye mahusiano ili kuzuia ongezeko la idadi ya vijana wanaoambukizwa virusi hivyo hapa jimboni Marsabit.
Qabale vilevile ametoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserekali katika kaunti ya Marsabit kuwapa msaada wa chakula watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi kwani wamepokea msaada mchache mno kutoka kwa serikali ya kaunti.