Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Hisia kinzani zimeibuliwa katika kikao cha umaa cha kutoa maoni kuhusiana mswaada wa kumbadua mamlakani naibu wa rais Rigathi Gachagua.
Baadhi ya wananchi ambao wamezungumza katika kikao hicho ambacho kimeandaliwa katika ukumbi wa kanisa Katoliki hapa mjini Marsabit, wametaja kuunga mkono ajenda ya kumtimua naibu wa rais kwa kile wamekitaja kwamba ni kukaidi mkubwa wake rais William Ruto.
Aidha baadhi yao wamepinga ajenda hiyo wakiitaja kama inayolenga tu kumtimua naibu wa rais kutokana naye kuzungumza ukweli.
Wameitaja hoja ya kumbandua itupiliwe mbali kwani sababu zilitolewa na bunge la kitaifa hazina misingi yeyote.
Wengine wao wametaja iwapo kuna hoja ya kumbandua yeyote mamlakani basi rais na naibu wake wanafaa wote kubanduliwa kwani chini ya uongozi wao hali ya maisha imekuwa ngumu zaidi sawa na visa vya ufisadi kuongezeka.
Aidha kwa wakati fulani vikao vya hivyo vya kutoa maoni vilisitishwa kutokana na migawanyiko ya maoni tofauti kutoka kwa wanaMarsabit.
Kwa upande wao viongozi wa jimbo hili walihudhuria hafla hiyo wakiongozwa na mwakilishi wa kike Naomi Jillo Waqo wametaja kwamba zoezi hili linalenga kumbandua naibu wa rais na ambaye kulingana naye hajakuwa akimuheshimu rais.
Naomi hata hivyo amekanusha kauli ya kwamba zoezi hilo linafanyika katika eneo bunge moja pekee hapa jimboni akitaja kuwa maeneo mengine pia yamehusika katika zoezi hilo.
Kwa upande wake mbunge wa Saku Dido Ali Raso amesema kuwa ipo hoja ya maeneo kusawazishwa katika ugavi wa rasilimali ili kuhakikisha kuwa kuna usawa kwa wananchi.
Aidha mtunga sheria huyo ametetea zoezi hilo akilitaja kama linalofaa katika kufanikisha mswaada wa kumbadua Gachagua mamlakani.