Afueni kwa wanafunzi 132 wa shule ya upili ya Goro Rukesa baada ya KNEC kuachilia matokeo ya mitihani yao….
January 21, 2025
GAVANA wa kaunti ya Marsabit Mohamud Ali amemtaka rais William Ruto kumaliza kero la ukosefu wa maji katika kaunti za ukanda huu wa kaskazini.
Gavana Ali akizungumza katika eneo la Archers Post kaunti ya Samburu leo Ijumaa amemtaka rais kuhakikisha kuwa mabwawa ya maji yaliyochimbwa au yanayochimbwa yakamilishwe kwa haraka katika muhula huu wa serikali ya sasa ili isadie wakaazi wa kaunti hizi kame.
Wakati uo huo Abshiro amekariri kuwa magavana kutoka eneo pana la kaskazini wanaunga mkono serikali ya Kenya Kwanza huku akishabikia mabadiliko ya uongozi ambayo yalishuhudia kufurushwa kwa aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua. Anasema hilo litahakikisha uwepo wa umoja wa taifa.