Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Kiu ya elimu inaonekana kuisakama idadi kubwa ya watu wazima katika kaunti ya Marsabit haswa kina mama ambao wanaonekana kutafuta huduma za masomo katika taasisi za elimu ya Gumbaru.
Kutokana na kiu na hitaji la baadhi ya kina mama kusoma ili kujitengemea kimaisha, idadi kubwa ya akina Mama imejisajili katika taasisi za elimu ya Gumbaru ya Turbi Pioneer iliyoko Turbi kaunti ya Marsabit.
Jebii kilimo ambaye ni waziri wa zamani ya jinsia amesema kuwa elimu ni chombo muhimu cha kuleta maendeleo na mabadiliko katika jamii.
Aidha Chebii ametaja kuwa elimu ya gumbaru itasidia wamama wengi katika kusaidia watoto wao katika swala la mtaala wa CBC.
Mbunge wa North Horr, Wario Adhe, amesema kuwa jamii za wafugaji kutoka eneo bunge lake wana fursa ya kupata masomo, iwe ya watoto au watu wazima, akisema kuwa hilo litasaidia kuboresha amani katika eneo hilo..
Hata hivyo, Hillary Halkano, ambaye ni mkaazi wa Turbi, ametaja kuwa wanaume wengi katika eneo hilo hawajisajili katika shule hizo kutokana na matumizi ya mihadarati, na hata wengi wao kuipa kipaumbele mifugo zao kuliko elimu.