Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Chifu wa eneo la Laisamis Agostino Supeer ametoa onyo kali kwa wazazi wanaopania kuwakeketa au kuwaoza watoto wao wakati wa likizo akisema kuwa watakaopatikana wakiendeleza uovu huo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya simu,chifu Agostino ameweka wazi kuwa baadhi ya wazazi hutumia kipindi cha likizo kuendeleza dhulma hizo dhidi ya wasichana huku wakizitaja kama tamaduni, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Aidha Chifu Agostino amewataka wazazi kuwajibika katika kipindi cha likizo na kuhakikisha kwamba watoto pia hawajiingiza katika utumizi wa mihadarati na dawa za kulevya huku akitoa onyo kwa wale wanaoendeleza biashara hiyo katika eneo hilo.