Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Chama cha kutetea maslahi ya walimu (KNUT) tawi la Marsabit kimechagua mwalimu Kula Lula Omar kuwa mwenyekiti wake mpya kwenye uchaguzi mdogo ulifanyika mjini Marsabit siku ya Jumamosi.
Kula sasa anajaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi na mumewe aliyeaga dunia mwanzoni mwa mwaka Huu.
Nafasi hiyo ilikuwa imevutia wagombeaji wawili ambao ni Kula Lula Omar na John Haro. Kula alishinda nafasi hiyo kwa kuzoa kura 104 dhidi ya 82 alizopata mwalimu Haro.
Katibu wa chama hicho cha KNUT kaunti ya Marsabit Rosemary Talaso ameambia kituo hiki kuwa kujazwa kwa nafasi hiyo kutahakikisha utendakazi bora wa chama hicho cha kutetea walimu.
Walimu wanachama kutoka kaunti zote ndogo za Marsabit ndio waliopiga kura.
Wakati uo huo ameirai wizara ya elimu nchini kushughulikia malalamishi ya walimu wanaosahihisha mitihani wanateta kuwa malipo Yao Ni kidogo ikilinganishwa na kazi wanayofanya.