Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
NA SAMUEL KOSGEI
Jamii zinazoishi kaunti ndgo ya Moyale na Marsabit kwa ujumla zimetakiwa kuendelea kuishi kwa njia ya Amani na ushirikiano ili kufanikisha maendeleo na uwiano.
Kauli hiyo imetolewa na Mohamednur Korme ambaye ni mwenyekiti wa muungano wa Amani Moyale na pia katibu wa muungano ya Amani ng’ambo ya Moyale Ethiopia na Moyale Kenya.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi ya kuendesha shughuli za Amani na shirika la Voluntary Service Oversees (VSO) Korme ameambia jamii za Marsabit kuiga mfano wa jamii za Moyale ambao tangu kumalizika kwa vita vya kijamii mwaka wa 2013/14 sasa wamekumbatia Amani ya kweli.
Korme anasema kuwa ofisi waliokabidhiwa itawafaa sana katika kuendesha shughuli zao za kila siku za kurai Amani kati ya jamii zote za Moyale. Anasema wanashirikiana na wenzao kutoka upande wa Ethiopia kuzima mchipuko wa mzozo wa kijamii.
Temesgen Tilaun ambaye ni msimamizi wa utekelezwaji wa miradi za VSO amesema kuwa ofisi iliopewa baraza la usalama za wazee itawafaa wazee hao wa Amani katika kuendesha shughuli zao ya kuleta jamii pamoja.
Aidha amekariri haja ya wazee hao kuhakikisha kuwa usalama unashuhudiwa kutoka pande zote mbili za Ethiopia na Kenya kwani pasipo na uwiano maendeleo yatakoma kuonekana.
Akina mama Moyale pia wameshabikia kujumuishwa kwa akina mama katika maamuzi ya Amani ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo akina mama hawakuhusishwa kwenye maamuzi ya kijamii.
Shemsia Abdulahi amesema kuwa akina mama wanasuluhu ya Amani na hivyo kuna haja ya kuhusishwa mara kwa mara.
Harakati hizo ya kuleta uwiano na usalama miongoni mwa jamii za Moyale zinaendelezwa na mashirika yasio ya kiserikali kama vile VSO, HODI, CDG chini ya ufadhili wa shirika la kimataifa la Austrian Development Agency ikishirikiana na serikali ya jimbo la Marsabit pamoja na serikali ya kitaifa.