Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Baadhi ya viongozi wa kidini nchini wamekosoa visa vya utekaji nyara nchini wakisema vinaendelea kuongezeka.
Wakiongozwa na Kiongozi wa dini ya Kiislamu Famau Mohamed Famau na Askofu wa kanisa Katoliki Dayosisi ya Malindi Willybard Lagho ambao kauli zao zimejiri kufuatia utekaji nyara wa raia wa Uturuki wamesema utekaji nyara utasababisha baadhi ya wanaozuru taifa hili kusitisha safari zao.
Famau na Lagho wamesema hulka hiyo ya utekaji nyara inaharibu sifa njema ya taifa hili na kutoa wito kwa serikali kuu kuweka mikakati ya kudhibiti visa hivyo vya utekaji nyara.
Wawili hao wameitaka serekali pia kuwahakikishia usalama wao raia wa kigeni pamoja na wa humu nchini na kuondoa wasiwasi kwao kutokana na idadi ya visa vya utekaji nyara ambavyo vinazidi kuripotiwa nchini.