County Updates, Diocese of Marsabit, Editorial, Local Bulletins, National News

BAADHI YA VIJANA WA KIZAZI KIPYA ALMAARUFU GEN ZS KATIKA MJI WA MARSABIT WATOA HISIA ZAO KUHUSISNA NA KAULI INAYOZAGAA KUWA HAWASAIDII WAZAZI WAO.

Na Naima Abdullahi,

Baadhi ya vijana wa kizazi kipya almaarufu Gen Zs katika mji wa Marsabit wametoa hisia zote kuhusisna na kauli inayozagaa kuwa hawasaidii wazazi wao.

Wakizungumza na Radio Jangwani vijana hao walilaumu ugumu ya maisha kama ya moja ya changamoto zinazopelekea wao kutowasidia wazazi.

Aidha baadhi ya Gen Z walilalama ya kwamba ukosefu ya fedha za kutosha na kumudu familia zao unachangia pakubwa katika kutosaidia wazazi wao huku wakiitaja gharama ya juu ya maisha pamoja na shinikizo la rika kama maswala mengine yanayowaadhiri.

Hata hivyo baadhi ya wazazi waliozungumza nasi wakiongozwa na mzee Guyo Bonaya amekitaja kizazi hicho kama kinachowatenga haswa baada ya kupata ajira.

Subscribe to eNewsletter