Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
HUKU taifa likiwa limezama kwenye mjadala wa mgogoro wa uongozi kati ya rais William Ruto na Rigathi Gachagua wito wa amani na utulivu unazidi kutolewa na viongozi wa kidini.
Askofu wa kanisa la kianglikana kaunti ya Marsabit Daniel Wario Qampicha ameirai pande zote mbili zinazozona kusitisha malumbano yao kwani hali tete nchini inasababisha kujivuta kwa maendeleo na hata kuvuruga utulivu wa jamii mbalimbali nchini.
Akizungumza na kituo hiki kwa njia ya kipekee, Askofu Qampicha amewataka wanasiasa kulegeza misimamo yao na kuzingatia kilio cha wakenya wanaopitia wakati mgumu.
Aidha amewataka viongozi nchini kuipa kilio cha wakenya kipaumbele badala ya maslahi yao. Anasema kuzidi kulumbana ina mathara mengi ikilinganishwa na faida za kibinafsi wanazopata wanasiasa.
Vile vile amewataka wakenya kutokubali kugawanywa na wanasiasa wachochezi kwani mara nyingi hawapiganii maslahi ya wakenya bali ni kujitakia makuu.
Wakati uo huo Qampicha ameonya na kuwataadharisha wanafunzi dhidi ya kujihusisha na udanganyifu kwenye mitihani ya kitaifa KCSE.
Qampicha ameambia shajara kuwa katika miaka ya nyuma, wanafunzi wamekuwa wakijihusisha kwenye udanganyifu wa mitihani suala analosema kuwa litaathiri maisha yao miaka ijayo.
Ameshutumu pia wazazi na walimu wanaounga mkono kufanyika kwa wizi wa mitihani akisema hilo litasababisha kupatikana kwa wataalamu warongo na wasiofuzu miaka ya baadaye.
Wakti uo huo amewatakia wanafunzi hao mafanikio kwenye mitihani ya kitaifa KCSE sawa na kuwatia shime wazazi kuwalinda watoto wao kwenye maadili mema haswa wapoelekea likizo ndefu ya mwezi wa December. Amewataka wanafunzi kuishi katika maisha ya Imani ya Mungu.