Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
ASKOFU wa kanisa la PEFA kaunti ya Marsabit Fredrick Gache Jibo amekosoa viongozi wa kisiasa nchini kwa kutoipa kipaumbele maslahi ya wakenya wanaopitia magumu kwa sasa.
Askofu Gache akizungumza na radio Jangwani amesema kuwa viongozi wakuu serikalini wanapigania maslahi yao kwa kutumia kiwango kikubwa cha pesa kulipa mawakili kwenye kesi ya kuzuia kubanduliwa kwa naibu rais Righathi Gachagua.
Gache ameambia shajara kuwa pesa nyingi zitatumika kulipa mawakili ilhali baadhi ya wafayakazi wa serikali wanapanga migomo kutokana malimbikizi au mishahara kuchelewa.
Wakati uo huo Askofu Gache amewataka viongozi wa kidini nchini kutokubali siasa ziendeshwe katika madhabahu ya Mungu. Amesema viongozi wa kidini wanafaa kudhibiti siasa kwenye maeneo ya mahubiri.
Ameongeza kusema kuwa mzozo wa uongozi nchini unaoshuhudiwa unatokana na mapuuza ya kuheshimu Mungu na kutoheshimiana kati ya viongozi nchini.
Kuhusiana na ongezeko la wizi wa kimabavu mjini Marsabit kiongozi huyo wa kidini amerai vijana kukoma kujihusisha na uhalifu kwani hilo anasema itakatisha maisha yao pindi serikali itakapotumia nguvu.